Maboresho ya kodi na mwingiliano wa matumizi ya serikali

MABORESHO ya kodi ni suala ambalo limekuwa kitovu cha majadaliano mengi yahusuyo uchumi katika miaka ya hivi karibuni, huku serikali pamoja na watunga sera wakijitahidi kujenga mfumo wa kodi ambao ni wa haki na unaofaa.

Sera ya fedha inayojumuisha kodi na matumizi ya serikali, ina nafasi kubwa kuimarisha utulivu wa kiuchumi huku ikiathiri kila kitu kuanzia mfumuko wa bei na ajira hadi katika huduma za umma na deni la taifa.

Kimsingi, kadiri serikali zinavyofanya kazi kuboresha miundo ya kodi, ndivyo uelewa wa namna mapato yanavyotolewa na kugawanywa unavyozidi kuwa muhimu.

Advertisement

Hofu ya umma
Mkazi wa Shinyanga, James TupaTupa anachangia mtazamo wake kuhusu uwazi katika matumizi ya serikali. Kwa mujibu wa TupaTupa, wafanyabiashara na wananchi wanataka uwazi kuhusu namna mapato ya kodi yanavyotumika.

Anabainisha kuwa, matumizi mabaya ya kodi si tu kwamba huondoa imani ya umma, bali pia hudhoofisha ukuaji wa uchumi. TupaTupa anasisitiza kuwa, mara nyingi kukosekana kwa muunganiko kati ya sera za kodi na vipaumbele vya matumizi ya serikali husababisha upungufu katika bajeti, huchochea ukopaji na kusababisha ufanisi duni katika
utoaji wa huduma muhimu za umma.

Mapato ya kodi hufadhili huduma mbalimbali za jamii ikiwamo miundombinu ya barabara na umeme.

Kwa ujumla, mpangilio mbaya wa sera za fedha hukwamisha ufanisi katika utawala na maendeleo ya uchumi.
Anasema wito wa kuboresha uwazi umepata mvuto mkubwa huku wananchi wakisisitiza uhalali wa kina zaidi  kuhusu namna serikali zinavyopanga fedha za umma.

Kadiri wasiwasi unavyoongezeka, umma unadai sera za kodi ziwiane zaidi na malengo ya taifa kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha kodi hazikusanywi tu, bali pia zinatumiwa kwa namna zinazofaidisha jamii.

Kwa mujibu wa watu mbalimbali, maboresho ya kodi hayawezi kupata ufanisi kamili hadi tu, makosa na uzembe katika matumizi ya umma yatakaposhughulikiwa kwanza. Kwamba, bila umakini katika namna matumizi ya serikali yanavyowiana na ukusanyaji wa kodi, maboresho hayatakamilika.

Ufuatiliaji huu unalenga kujadili kwa kina namna matumizi ya serikali yanavyoathiri miundo ya kodi, kutambua changamoto zinazoikabili serikali inapokagua mifumo ya matumizi na kutoa mapendekezo kwa watunga sera.

Kadiri uhusiano baina ya ukusanyaji kodi na matumizi ya serikali unavyokuwa muhimu kwa taifa kifedha pamoja na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuelewa na kuboresha mabadiliko hayo ni muhimu ili kuhakikisha kuna  mustakabali endelevu na wenye usawa.

SOMA: Wadau wa kodi wataka haki mizozo na TRA

Kwa kuingia kwa kina zaidi katika mazungumzo haya, makala haya yanatarajia kutoa maoni muhimu kuhusu namna
sera za fedha zinavyoweza kuboresha kwa utulivu wa muda mrefu wa kiuchumi na kwa ustawi wa umma.

Mapato dhidi ya matumizi
Kimsingi, serikali hutegemea mapato ya kodi kufadhili huduma mbalimbali za jamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, miundombinu na usalama wa umma.

Ufanisi wa mfumo wa kodi katika taifa hufungamana kwa karibu na namna unavyoendana na vipaumbele vyake vya
matumizi. Kwa maana hiyo, uwiano kati ya mapato yatokanayo na kodi na matumizi ya serikali, ni muhimu kwa ajili ya usimamizi endelevu wa fedha na utoaji wa huduma bora kwa umma.

Mtaalamu wa kodi kutoka Lanarkhire Kaskazini nchini Scotland, Lachlan Thomson anazungumzia makubaliano ya kimataifa akisema ufanisi wa mfumo wa kodi kwa taifa huhusishwa na vipaumbele vyake vya matumizi.

Anasisitiza kuwa, mifumo ya kodi isipoendana na mahitaji ya matumizi ya taifa husababisha kukosekana kwa usawa wa fedha. Mwanauchumi anayeishi Mwanza, Robert Msuya anaunga mkono maoni ya Thomson anayesema upungufu katika ukusanyaji kodi mara nyingi husababisha upungufu katika bajeti.

Hali hii hufanya serikali ilazimike kukopa, jambo linaloongeza deni la taifa na kuweka mzigo kwa vizazi vijavyo.
Kuonesha ugumu wa suala hili, Thomson anarejelea hali ya Uingereza, ambako mzigo wa kodi umeongezeka katika
miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa makisio yake, ifikapo 2027- 2028 mzigo wa kodi wa Uingereza utafikia asilimia 38.3 ya Pato la Taifa
ambalo ni ongezeko kubwa kutokana na uamuzi ya sera na changamoto za kiuchumi zinazoendelea.

Anasema hili likitokea, mzigo huo mkubwa wa kodi pamoja na ukuaji duni wa uchumi (pamoja na ukuaji wa Pato la Taifa la Uingereza katika robo ya mwisho ya mwaka uliopita kuwa asilimia 0.1 tu), utaibua hofu ya kuingia kwenye kitanzi.

Hali kama hiyo ambapo ukuaji mdogo husababisha kuongezeka kwa kodi inaweza kusababisha kudorora kwa uchumi. Thomson anaonya kuwa, uwepo wa kodi kubwa kama inavyoonekana katika mfano wa Uingereza, unaweza kukwamisha ukuaji wa uchumi, kukatisha tamaa uwekezaji na kulemea walipakodi.

Utozaji kodi huu mkubwa kupita kiasi unaweza kusababisha madhara ya kupungua kwa shughuli za biashara na kupunguza matumizi ya watumiaji, hivyo kudhoofisha uhimilivu wa uchumi wa nchi. Kwa msingi huo, kuwapo kwa uwiano sahihi kati ya mapato ya kodi na matumizi ya serikali ni muhimu kwa manufaa ya muda mrefu ya uchumi nchini.

Mfumo unaochochea uendelevu wa kifedha na utoaji wa huduma bora kwa umma, unapaswa kuhakikisha serikali
zinaweza kutimiza wajibu bila kuzuia ukuaji wa uchumi na bila kutupa mzigo kwa wananchi.

Mapato kama asilimia yaPato la Taifa
Mtaalamu wa masuala ya kodi aishiye Arusha, Jane Mollel anasema mapato ya kodi kama  asilimia ya Pato la Taifa (GDP) ni kiashiria muhimu cha uwezo wa kifedha wa nchi na afya ya uchumi kwa ujumla. Anasema katika Afrika,
Kusini mwa Jangwa la Sahara, uwiano huu hutofautiana kwa kiasi kikubwa kutoka nchi moja hadi nyingine ukiakisi tofauti baina ya sera za kodi, taratibu za utekelezaji na miundo ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, wastani wa uwiano wa kodi kwa Pato la Taifa katika kanda ni takribani asilimia 15,
chini ya wastani wa kimataifa wa karibu asilimia 34 unaozingatiwa na nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano
wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).

Mollel anasema Afrika Kusini yenye uwiano wa kodi kwa Pato la Taifa wa takribani asilimia 26, inaonesha wigo
mpana zaidi wa vyanzo vya kodi na mbinu bora za ukusanyaji, hivyo kuruhusu uwekezaji mkubwa wa umma katika miundombinu, huduma za afya na programu mbalimbali za kijamii.

Kinyume chake, uwiano wa kodi kwa Pato la Taifa nchini Nigeria unasimama katika asilimia 10.8 tu ambayo ni moja ya viwango vya chini zaidi katika kanda. Kwa mujibu wa Mollel, hii ni ishara ya changamoto za kimuundo kama ulipaji mdogo wa kodi, utegemezi mkubwa wa mapato ya mafuta na kuwapo sekta kubwa isiyo rasmi ambayo haitozwi kodi.

Anasema tofauti hizi zinaonesha hitaji muhimu la maboresho ya kodi katika mataifa mengi ya Afrika yanayolenga
kupanua wigo wa vyanzo vya kodi, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na kuongeza uwazi katika matumizi ya serikali ili kujenga imani ya umma.

Kuimarisha maeneo haya kutawezesha serikali kupata uzalishaji endelevu wa mapato kwa ajili ya maendeleo ya taifa
bila kulemea walipa kodi. Ufanisi na Usawa Wadau mbalimbali akiwemo mwanauchumi wa Uganda, Louis Mugume wanasema ugawaji wa mapato ya kodi una nafasi muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na usawa wa kijamii.

Matumizi bora ya serikali yanaweza kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa kuwekeza katika sekta muhimu kama miundombinu, elimu na teknolojia hivyo kukuza uzalishaji wa ajira na uvumbuzi.

Hata hivyo, Mugume anaonya kuwa, kutokuwapo kwa ufanisi yaani kuwapo kwa vikwazo vya usimamizi, mgawanyo mbaya wa fedha na hata kuongezeka kwa gharama za uendeshaji ni mambo yanayoweza kudhoofisha manufaa kusudiwa ya sera za kodi.

Akitumia uzoefu wake wa kufanya kazi na Marehemu Emmanuel Tumusiime-Mutebile, mwanauchumi mashuhuri nchini Uganda na Gavana wa zamani wa Benki ya Uganda, Mugume anarejea utafiti wa kutathmini ufanisi wa matumizi ya serikali barani Afrika.

Utafiti huo ulibainisha kuwa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na usimamizi duni wa matumizi ya umma hali inayosababisha matokeo duni kijamii na kiuchumi. Idadi kubwa ya watu bado inakabiliwa na umaskini na uhaba wa chakula hali inayoonesha hitaji la haraka la sera zilizo wazi na zenye ufanisi zaidi kifedha.

Hoja ya Mugume inaungwa mkono na Hassan Hassan ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kodi aishiye Mbeya.
Hassan anadokeza kuwa, uzembe katika usimamizi wa kodi si barani Afrika pekee, bali pia umeenea katika nchi zilizoendelea kiuchumi.

Anatoa mfano wa Uingereza ambapo Ofisi ya Kitaifa ya Ukaguzi iliripoti ongezeko la asilimia 15 ya gharama za
usimamizi wa kodi kati ya mwaka 2019 na 2024 ambayo ni nyongeza ya Pauni milioni 563.

Ugumu wa mfumo wa kodi wa Uingereza na kuongezeka kwa idadi ya walipa kodi umesababisha gharama kubwa za utekelezaji wa kanuni na sheria za kodi kwa biashara inayokadiriwa kuwa ya Pauni bilioni 15.4 kila mwaka.

Hassan anasema uzembe huo si tu kwamba unasumbua rasilimali za umma, bali pia unaondoa imani katika mfumo wa kodi na kufanya maboresho ya kodi kutokuwa na ufanisi katika kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kiuchumi na kijamii. Kimsingi, suala la usawa katika utozaji kodi lilikuwa mada maarufu miongoni mwa waliotoa maoni.

Hidaya Hussein wa Pemba anasisitiza kuwa, utozaji wakodi inayoongezeka umeundwa ili kugawanya tena mali na kupunguza tofauti ya kipato kwa kuweka viwango vya juu vya kodi kwa wale wenye mapato makubwa. Anasema manufaa haya mara nyingi huathiriwa na matumizi ya umma yanaposhindwa kusaidia ipasavyo vikundi vya kipato cha chini kupitia programu za kijamii na huduma muhimu.

Hussein anasisitiza kuwa, uwepo wa sera za kodi zinazoendana na matumizi ya serikali ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi jumuishi na uimara wa kijamii. Mshauri wa masuala ya fedha aliyehamia Songea hivi karibuni, Harry Samwel anatumia nchi ya Nigeria kama mfano wa mwingiliano baina ya sera ya kodi na matumizi ya serikali.

Januari 2025, Serikali ya Nigeria ilipendekeza maboresho makubwa ya kodi yanayolenga kuongeza ukusanyaji wa mapato na kupunguza mfumuko wa bei.

Wachambuzi mbalimbali nchini wanasema maboresho haya yanapaswa kuwa maradufu kwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) hadi asilimia 12.5 ifikapo 2026 huku yakitoa msamaha kwa bidhaa muhimu kama chakula na dawa kuepusha mzigo kwa kaya zenye kipato cha chini.

Wanaounga mkono sera hiyo wanasema urekebishaji huo utaimarisha ulipaji kodi na kuoanisha Nigeria na viwango
vya kodi vya kimataifa. Kwa upande wao, wakosoaji wa sera wanasema ongezeko la VAT lisipoambatana na matumizi sahihi ya umma yenye uwazi, linaweza kuzuia matumizi na ukuaji wa viwanda na hatimaye kukwamisha manufaa ya kifedha.

Upatikanaji wa huduma za maji safi na salama kwa karibu ni moja ya matunda yatokanayo na kodi.

Mitazamo hii inasisitiza hitaji muhimu la kuwapo sera za kodi ambazo si tu zimeundwa vizuri, bali pia zinawiana kwa karibu na matumizi ya serikali yaliyo wazi na yenye ufanisi. Kimsingi, bila usimamizi mzuri wa fedha, hata maboresho bora zaidi ya kodi yanayokusudiwa yatakuwa katika hatari ya kushindwa kuleta manufaa yanayoonekana kwa uchumi na jamii kwa ujumla.

Ulinganisho wa kimataifa
Mikakati ya kifedha katika nchi mbalimbali inatoa funzo muhimu katika kuwianisha ukusanyaji wa mapato ya kodi
na matumizi ya umma ili kuchochea ukuaji wa uchumi na usawa wa kijamii. Nchi kama vile Sweden, Singapore na Ujerumani zina mbinu mbalimbali zinazoonesha njia kadhaa zinazoweza kutumiwa na serikali kudhibiti kodi na matumizi ili kupata uendelevu wa kifedha na ustawi wa umma.

Sweden
Mtaalamu kutoka Lanarkhire Kaskazini anasema, “Uwiano wa juu wa kodi kwa Pato la Taifa wa Sweden wa asilimia 44.3 mwaka 2022 unafadhili kwa kina mfumo wake wa ustawi na kuhakikisha kuna elimu bila malipo, huduma za afya kwa wote pamoja na mitandao thabiti ya usalama wa kijamii.”

Anasema mfumo wake wa kodi inayoongezeka wenye kiwango cha juu cha kodi wa asilimia 57.1, hugawanya utajiri na kupunguza ukosefu wa usawa.  Licha ya kiwango kikubwa cha kodi, Sweden imedumisha imani kwa umma kutokana na usimamizi wake wa wazi huku Ofisi ya Kitaifa ya Ukaguzi ya Sweden ikihakikisha kuna matumizi sahihi ya fedha.

“Mgawo mzuri wa mapato ya kodi nchini Sweden hutokea katika ya makadirio ya juu zaidi ya uidhinishaji wa sekta ya umma barani Ulaya,” anasema. Mbinu hii imesaidia ukuaji thabiti wa uchumi, ambapo Pato la Taifa kwa kila mtu
lilikuwa Dola za Marekani 58,000 mwaka wa 2022 na kuthibitisha kwamba, utozaji kodi unaposimamiwa vyema
huchochea usawa wa kijamii na utulivu wa kiuchumi.

Singapore

Jane Mollel anawasilisha mbinu tofauti ya nchini Singapore ya kutoa huduma bora za umma na mzigo mdogo wa kodi. Uwiano wa Kodi ya asilimia 44.3 kwa Pato la Taifa wa Sweden hufadhili mipango mingi ya ustawi wakati Singapore yenye asilimia 13.6 pekee, inategemea matumizi bora na uwekezaji wa kimkakati kudumisha uimara wa kiuchumi.

Mollel anasema, “Ruzuku zinazolengwa za Singapore na usimamizi makini wa fedha hupunguza upotevu na kuhakikikisha huduma muhimu zinaendelea kupatikana.” Mtindo huu ni tofauti na uchumi wa kodi kubwa
unathibitisha kuwa, matumizi yaliyopangwa sawia yanaweza kuendeleza ukuaji wa uchumi bila kodi kubwa.

Mbinu hizo zote zinaonesha kuwa, sera madhubuti ya fedha haihusu viwango vya kodi pekee, bali pia namna mapato yanavyodhibitiwa. Mtazamo wa usawa wa kijamii wa Sweden na mtindo wa kiuchumi wenye ufanisi wa Singapore hutoa somo muhimu kwa watunga sera wanaotafuta mikakati endelevu ya kodi na matumizi.

Ujerumani
Wakati Sweden, Singapore na Ujerumani zinafanya vizuri katika usimamizi wa fedha, mikakati yao tofauti inachochea mjadala kuhusu uwiano sahihi baina ya kodi, matumizi ya umma na ukuaji wa uchumi.

Mwanauchumi nchini Uganda, Louis Mugume anasema, “Ujerumani ipo kati yaani, haipo katika mfumo wa kodi ya juu kwa ustawi wa watu wa Sweden, wala haipo kwenye mfano wa sera ya Serikali ya Singapore badala yake, badala yake inaendeleza msingi thabiti wa kisekta huku ikiweka mzigo wa wastani wa kodi.”

Kwa uwiano wa kodi wa asilimia 38.1 kwa Pato la Taifa, Ujerumani inakaa kati ya asilimia 44.3 ya Sweden na asilimia 13.6 ya Singapore ikiweka usawa baina ya sera rafiki za biashara na miundombinu ya kijamii.

Kiwango chake cha kodi cha asilimia 15 kwa mashirika kinahimiza uwekezaji huku matajiri wakilipa hadi asilimia 45 kufadhili sekta muhimu kama elimu na nishati jadidifu, pamoja na kuchangia kupungua kwa ukosefu wa ajira barani
Ulaya (asilimia 3 mwaka 2022).

Hata hivyo, sheria kali ya Ujerumani inayozuia deni jipya inabaki kuwa mgawanyiko. Mawakili wanaisifu kama ya nidhamu ya fedha huku wakosoaji wakisema inadhoofisha vichocheo vya uchumi. Cha kujiuliza ni je, ni mbinu gani inayofanya kazi vizuri zaidi? Mfumo wa kodi kubwa, mfumo wa huduma za juu wa Sweden? Mfumo wa kodi ya ndogo wa Singapore wenye ufanisi mkubwa?

Sheria ya kusawazisha Mawazo ya wataalamu yanaweka wazi zaidi suala la kuoanisha sera za kodi na matumizi bora ya serikali kuwa si tu kurekebisha nambari, bali kufanya uchaguzi makini unaochochea ukuaji wa uchumi na usawa wa kijamii.

Nchi kama Sweden, Singapore na Ujerumani zinathibitisha kuwa mafanikio hutokana na uamuzi wa kimkakati na si tu kuongeza kodi au kupunguza bajeti. Kwa Afrika na Tanzania kipekee, dau ni kubwa. Masomo haya ya kimataifa si ya hiari, bali muhimu sana.

Suala la msingi hapa si kama mifano hii inaweza kufanya kazi, bali kwa kasi gani tunaweza kukabiliana nayo. Je, watunga sera wanaweza kutenda kwa ujasiri mkubwa kuvunja uzembe uliopo na kuchochea mabadiliko ya kweli?
Ukweli usiofurahisha ni kwamba bila mabadiliko makubwa, Afrika itazidi kubaki katika hatari ya kurudi nyuma.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *