Mhandisi Ndolezi aanza ziara Kigoma Kusini

WAZIRI Kivuli wa ACT Wazalendo Ofisi ya Waziri Mkuu -Bunge Sera Vijana Kazi na Ajira Mhandisi Ndolezi Petro ameanza ziara katika Jimbo la Kigoma Kusini ya kuzifikia kata 16 na vijiji 61 mkoani Kigoma.

Katika kikao alichofan ya jana na Kamati ya Uongozi ya Jimbo, Mhandisi Ndolezi Petro amewakabidhi vitendea kazi viongozi wa jimbo vitavyoweza kusaidia wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Advertisement

Vitendea kazi hivyo ni pamoja na mihuri ya makatibu tawi kwenye vijiji vyote 61 na kata 16, amekabidhi pia Stamp Pad 72 za wino wa mihuri, bendera 32 , vipeperushi 300 vya ratiba ya uchaguzi.

SOMA: Ndolezi ashauri nguvu zaidi kwenye teknolojia

Vifaa vyote vimepokelewa na viongozi wa Jimbo la Kigoma Kusini wakiongozwa na Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Yakubu Nzigamiye.

Ndolezi pia amewataka viongozi waendelee kufanya kazi ya kuhamasisha Wanachama wa jimbo hilo kujiandikisha na kuhakikisha wagombea wenye sifa na kukubalika wanapata nafasi ya kugombea na kuweza kupata fursa ya kuwatumikia Wananchi.

SOMA: Ndolezi: Kunahitajika Baraza la Vijana la Taifa

Waziri Kivuli Mhandisi Ndolezi Petro amemtaka Mkurugenzi wa Wilaya ya Uvinza kutoingilia uchaguzi kwa nia ya kuvuruga.

“Tayari kuna viashiria vya nia isiyo njema juu ya mawakala kuapa ametoa ratiba ya kushtukiza na wengine baadhi ya maeneo ya kata waliambiwa waende Octoba 11, 2024 siku ya uandikishaji hii si nia njema”.amesema Mhandisi Ndolezi.

Ametoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Kigoma Kusini kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa .