Wananchi Itimila wasifu mfumo wa kifuta jasho

SIMIYU: Wananchi wa vijiji vya Nyantugutu, Lung’wa na Nding’ho vya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wameipongeza Serikali kwa kuunda na kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za wanyamapori wakali na waharibifu ambao umerahisisha malipo ya kifuta jasho/machozi pindi madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu yanapotokea kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ndi’hgo, Salome Kambona katika mkutano wa hadhara wa kuelimisha wananchi namna ya kukabiliana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu uliofanyika kijiji cha Ndi’hgo ,Wilaya ya Itilima leo Oktoba 9, 2025.
“Tunaishukuru Serikali kwa mfumo huu ambao ndani ya siku saba mwananchi atatakiwa awe ametoa taarifa ya madhara yaliyotokana na mnyamapori ili aweze kulipwa,” amesema Salome.
Naye, Mkazi wa Kijiji cha Nyantugutu, Mosses Saguda amesema mfumo wa PAIS umepunguza urasimu na usumbufu wa malipo.
“Tunaishukuru Serikali kwa utaratibu mpya wa mfumo wa malipo ya kifuta jasho/machozi kwani hauna usumbufu wowote na tunalipwa kwa simu au benki tofauti na awali tulikuwa tunakaa mwaka bila kulipwa,”amesema Saguda.
Aidha, ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa malipo ya kifuta jasho kwa wananchi wanaoharibiwa mazao yakiwa ghalani.
Akizungumza kuhusu elimu hiyo kwa wananchi, Ofisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Nassoro Wawa amesema matarajio ya Serikali baada ya mafunzo hayo ni kwamba wananchi wamepata uelewa jinsi ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na kujua sheria, kanuni na taratibu za kufuata ili kumiliki nyara za Serikali.
“Pia nimewaeleza wananchi kuwa sheria zinaruhusu kuwekeza katika sekta ya wanyamapori hususan kuanzisha bucha za nyamapori, bustani, mashamba na ranchi za wanyamapori ili waweze kujipatia vipato,”amesisitiza Wawa.
Elimu hiyo imetolewa mkoani humo kufuatia matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo, fisi, mamba na viboko.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com